The Color of Life – book launch
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka vijana kutumia muda wao kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu badala ya kupoteza muda wao mwingi katika mitandao ya kijamii kwakuwa kusoma vitabu ndiyo msingi mzuri wa elimu.
Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizindua Kitabu cha “The Colour of Life”; kilichoandikwa na Mwandishi Bi. Ritha Tarimo ambapo katika hotuba yake aliyoitoa mbele ya wageni waalikwa amesisitiza suala la vijana kujenga utamaduni wa kupenda kusoma vitabu ili kukuza elimu yao.
Mhe. Mwakyembe ameeleza kuwa, baadhi ya vijana siku hizi wamekuwa wakitumia muda wao mwingi katika mitandao ya kijamii badala ya kujisomea, hivyo amewashauri wajifunze kutoka kwa Mwandishi wa Kitabu hicho ili waje kuwa waandishi hodari wa kutegemewa na Taifa. Sambamba na rai hiyo, Waziri Mwakyembe amempongeza Bi. Ritha Tarimo kwa juhudi zake kubwa na maarifa katika kutunga na kuandika kitabu hicho ambacho amesema kuwa
kitabu hicho ni kizuri na kina maudhui mazuri kwa vijana hususani
wanafunzi, hivyo ameitaka jamii kumuunga mkono kwa kukisoma ili jamii ipate kuelimika.
“Ukimkuta mtu kama Ritha Tarimo anaandika kitabu katika kipindi hiki ambapo vitabu vinaonekana kuondolewa kwasababu ya maendeleo ya teknolojia, ni vema kumpa moyo na kumuunga mkono kwakuwa
yeye ametuonyesha Watanzania kuwa hata sisi tunaweza, na kitabu hiki
niwaambie ukweli kina maudhui ya kumtia moyo kijana ya kutokata tamaa katika maisha”; alisema Dkt. Mwakyembe.
Leave a Comments